Msanii Billnass amechora tattoo ya kwanza kwenye mwili wake, ambapo ameeleza kuwa imempatia maumivu makali.
Kupitia post yake aliyoweka katika mtandao wa Instagram Billnass ameandika kwamba "Tattoo yangu ya kwanza, ni stori ndefu inauma sana, na nampenda yeye".
Baada ya kuandika hivyo maswali yakawa mengi kupitia baadhi ya comments za mashabiki na wasanii wengine kumuuliza ni aina gani ya tattoo ameichora.
Sasa ukweli kuhusu jina la mchoro wa Tattoo hiyo amemalizana nao Nandy, ambaye kupitia mtandao wa Snapchat amemrekodi Billnass video fupi wakati anachora huku na kuandika, "Siwezi kuamini hili jina langu litakuwa kwenye mwili wake milele".
Kupitia post hiyo aliyoweka Nandy inathibitisha kuwa Billnass amechora tattoo ya jina la msanii huyo, ambaye inadaiwa kuwa wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.