F Corona yakwamisha safari ya Hussein Machozi kurudi Tanzania | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Corona yakwamisha safari ya Hussein Machozi kurudi Tanzania


Msanii Hussein Machozi anayeishi Italia amesema hawezi kurejea Tanzania kwa sasa kwa kuwa nchi hiyo pia ina maambukizi ya virusi vya corona.

Machozi yupo Italia ambako zaidi ya watu 13,000 wamefariki dunia kwa corona hadi leo jioni. Tanzania walioambukizwa ugonjwa huo ni  20, wawili wamepona na mmoja amefariki dunia.

“naishi roho yangu iko mkononi, nimekata tamaa sijui kama nitarudi mzima. Sina amani najaribu kuzoea hali halisi, kiukweli matumaini ya kupanda ndege siku moja nirudi nyumbani kama nilivyokuwa nafanya sidhani,  hali ni mbaya.”

Amesema mahitaji muhimu wanapata kwa njia ya simu, “au baadhi ya maduka makubwa ambayo wanaingia watu wawili tu.”

Msanii huyo amefananisha agizo la kutakiwa kukaa ndani na mtu aliyeko jela.