Jeshi la Uganda kuingia mtaani kudhibiti vitendo vya Polisi vya kuwanyanyasa Wananchi

Jeshi la Wananchi Uganda limeanzisha kikosi kazi ambacho kitakuwa kinazunguka mitaani usiku ili kuhakikisha udhibiti wa Watu kutembea usiku unafanyika bila kuvunja haki za Binadamu, hatua hii inakuja kufuatia malalamiko kuwa baadhi ya Polisi na mgambo wanawanyanyasa Wananchi.

Hatua ya Jeshi la Wananchi Uganda kuingia mtaani kudhibiti vitendo vya Polisi na mgambo kuwanyanyasa Wananchi inakuja wakati Shirika la Kutetea Haki za Binadamu, likiwa limeitaka Uganda kuhakikisha Askari wake wanajiepusha kutumia nguvu kutekeleza hatua za kukabiliana na corona.