Na Thabit Madai, Zanzibar.
Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuelimisha waumini wao kuhusu kujikinga na maambukizi ya corona
Akizungumza na mapadri,wachungaji na maimamu wa miskiti katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika ukumbi wa halmashaur kinduni mkuu wa wilaya ya kaskazin B Rajab Ali Rajab amesema viongozi hao wana nafasi kubwa kutokana na ukaribu uliopo na waumini wao
Amesema licha ya wilaya hiyo kuwa salama hadi sasa lakini bado IPO haja ya kuendelea kuelimishana ili jamii iendelee kujikinga na ugonjwa huo
Hata hivyo bwana Rajab amewataka viongozi hao kuliombea taifa pamoja na ulimwengu kwa ujumla ili uginjwa huo uweze kuondoka na kuondoa taharuki iliopo katika jamii
Aidha amewataka viongozi hao kufupisha mahubiri na kusoma sura fupifupi ili kwenda sambamba na maagizo ya serikali kuhusu katazo la mikusanyiko ya watu
Nao viongozi hao wameiomba ofisi ya mufti kuangalia kwa kina kama upo uwezekano wa misikiti isiyokuwa na sifa ya kusaliwa sala ya ijumaa isaliwe sala hiyo katika kipindi hiki li lile lengo la kukaa mita moja baina ya mtu na mtu iweze kutekelezwa
Hata hivyo wamemuhakikishia mkuu huyo wa wilaya kuwa watatekeleza kwa vitendo Yale yote waliyoagizwa ili kufikia malengo ya serikali katika mapambano dhidi ya corona