F BAKWATA Tanga yatoa siku 3 kwa watakaokiuka maelekezo ya serikali ya kujikinga na corona wakati wa swala | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

BAKWATA Tanga yatoa siku 3 kwa watakaokiuka maelekezo ya serikali ya kujikinga na corona wakati wa swala


Na Rebeca Duwe, Tanga


Baraza la waislamu Tanzania BAKWATA  wilaya ya Tanga imesema haitawavumilia baadhi ya waislamu wanaokiuka utaratibu na maekezo ya Serikali kuhusiana  tahadhari ya juu ya ugonjwa Covid 19  ambao kwa sasa unaitesa Dunia nzima na Tanzania kwa ujumla .

Hayo aliyasema Shekh mkuu wa wilaya ya Tanga  Alhaji Mohamedi Ally Kombora ,wakati akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya ofisi Bakwata  Mkoa wa  Tanga  kwamba wapo waislamu wanaopuuza maigizo ya serikali na endapo wataendelea kupuuza watafungiwa misikiti  hayo ambayo bado wanaendelea na mzaha.

Aidha alisema kuanzia leo hii watapewa siku tatu tu za kujirekebisha ili wafuate maelekezo ya serikali  ya kuacha nafasi ya mita moja baina ya mwingine na kuvaa barakoa na kuzingatia matumizi ya vitakasa mikono ili kuweza kujikinga na ugonjwa corona .

 “Wapo baadhi waislamu wanatupa masikitiko makubwa mno kwani wanapuuza maelekezo ya serikali katika kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao wenywe   hivyo wao kama  Baraza hawatavumilia kabisa kuona hiyo hali inaendelea.”alisema Alhaji Kombora.

Sambamba na hayo amewaomba waislamu wote kuwa mfano wa kuigwa kwa kuzingatia maelekeo ya wataalamu wa Afya na serikali kwa ujumla ili kuweza kujikinga na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Corona  ambao unaendelea kuasambaa kwani namna moja wapo ya kutokusambaa ni kutekeleza  maelekezo  hayo yanayotolewa.



Alisema kwamba wale watakaoendelea kupuuza maelekeza hayo watachukuliwa kali ikiwemo kufungiwa misikitiki yao mara baada ya siku tatu  walizokubaliana wao kama baraza na kwamba ipo kamati maalumu ya kuangalia utaratibu huo wakati ibada  ili kuhakikisha wanazingatia maelekezo.

 Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Bakwata Mwadini Haji Mwadini  aliwasisitiza waislamu wote kuzngatia  utaratibu wote uliowekwa na serikali lakini waweze kuwasikiliza viongozi wao wa ngazi ya juu wanaowaelekeza na kuwa wajibu wa kujikinga maambukizi ya ugonjwa Corona.

 Aliongeza kusema waislamu wawe mfano wa kuigwa wasisiburi mpaka kamati hiyo iliyoundwa kuipta kila msikiti ianze kufanya kazi badala yake wahakikishe wanaangalia usalama wao ili kujiepusha na msongamano ndani ya ibada zao.