F Dkt. Kawambwa akabidhi ndoo za maji tiririka | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Dkt. Kawambwa akabidhi ndoo za maji tiririka


Na Omary Mngindo, Bagamoyo


MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Dkt. Shukuru Kawambwa, amegawa ndoo 15 za maji tililika na sabuni zake, kwa ajili ya kunawa mikono kwa wakazi wa Kata za Dunda, Nianjema na Magomeni.

Hatua ya Mbunge huyo ni muendelezo wa mapambano dhidi ya maamukizi ya  ugonjwa wa Corona, ambao mpaka sasa bado wataalaamu wanaendelea kuumuza vichwa kuhusiana na upatikanaji wa dawa yake, ili wananchi waweze kuhepukana na ugonjwa huo.

Akiwa katika ziara maalumu iliyopitia vijiwe mbalimbali vya madereva wa pikipiki na maeneo ya masoko, Dkt. Kawambwa aliwatahadharisha wafanyabiashara wakiwemo wateja, wanaofika maeneo hayo kupata mahitaji mbalimbali, kwamba Corona bado ni hatari.

Aidha, Dkt. Kawambwa amewataka waendesha pikipiki kuhakikisha abiria zao wananawa vizuri mikono kwa kutumia maji tiririka na sabuni hizo, kabla ya kupanda kwenye vyomvo hivyo, kwani kwa kufanya hivyo kwa kiasi kikubwa watajiepusha na maambukizi hayo.

"Vijana wangu waendesha pikipiki na wafanyabiahara hakikisheni mnachukua tahadhari kubwa kuhusu ugonjwa huu, ili muweze kujikinga wenyewe binafsi sanjali na familia zenu nyumbani" Alisema Dkt. Kawambwa.

"Tunaona ambavyo maambukizi yanavyoendelea siku hadi siku, kwa nini nawe usiunge mkono juhudi za mheshimiwa Rais Dkt. John Maghufuli na viongozi mbalimbali zinazotuhimiza tupambane ili tunabaki salama?," Alihoji mbunge huyo.

Alisema ameongea na Wahisani waliowahi pia kusaidia kufanya operesheni ya macho bure, ambao ni Bilal Eye Camp ili nao waone umuhimu wa tahadhari, ambapo wamekubali kutoa ndoo za maji na sabuni ili zitumike kunawa mikono.

Dkt. Kawambwa amewatahadharisha juu ya namna ya kukaa kwa kupena nafasi kidogo kutoka mtu mmoja na mwingine, ikiwa ni kujikinga zaidi na maambukizi hayo ya ugonjwa huo hatari.

Kwa upande wao madiwani wa viti maalum Shumina Rashidi na Apsa Kilingo, wamewataka wafanyabiashara kwenye Kata hizo kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wanashinda vita dhidi ya Corona.

Nao Madiwani wa Kata za Nianjema Abdul Pyallah na wa kata Dunda Dickson Makamba, kwa upande wao wamemshukuru na kumpongeza Mbunge Dkt. Kawambwa, kwa kufanikisha zoezi hilo muhimu.

Wakizungumza baada ya kupokea misaada hiyo, viongozu katika maeneo hayo wamemshukuru Mbunge huyo kwa juhudi zake za kuwajili wananchi wake, hasa katika kipindi hiki cha ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona.