Na Timothy
Itembe Mara. HALMASHAURI
ya Rorya mkoani Mara jana katika Baraza la madiwani wamepokea vifaa vya
Sanitizer kutoka kikundi cha Rorya Forum ikiwa ni kuunga juhudi za Serikali
katika kupambana na ugonjwa hatari wa Corona. Akipokea
vifaa hivyo kwa ajili ya halmashauri Mwenyekiti,Albeth Machiwa alitumia nafasi
hiyo kushukuru kikundi hicho ambapo alisema kuwa Chupa moja ina uwezo wa kuokoa
uhai wa Mtu. “Niwashukuru
Ndugu zangu kwa msaada mliutoa ndani ya halmashauri yetu kwa hali hiyo milango
ipo wazi kwa wadau wengine wa maendeleo kuja na kushirikiana nasi katika
shuguli za maendeleo vifaa mlivyo toa vina mchango mkubwa katika halmashauri
yetu ambapo Chupa moja ina uwezo wa kuokoa uhai wa Mtu katika kufanya hivyo ni moja ya maendeleo kwa watu wa Rorya
na Tanzania kwa ujumla “alisema Machiwa. Mmoja wa
kikundi hicho,George Nyamasi kwa niaba ya
wenzake alisema kuwa kindi hicho kimewiwa na maendeleo ya Tanzania katika
kupambana na ugonjwa wa Corona ambapo wametoa Sanitizer kwa watumishi wa Hospitali,Vituo
vya Afya na Zahanati waliopo wilayani hapo ilikujikinga na COVID 19. Nyamasi
aliongeza kuwa vifaa walivyokabidhi Halmashauri ya Rorya vina dhamani ya zaidi
ya shilingi milioni moja na kuwa watendelea kutoa misaada katika halmashauri
hiyo kulingana na jinsi watakavyokuwa
wanabarikiwa na Mwenyezi Mungu. Mganga mkuu
wa halmashauri hiyo,DR Peter Mkenda aliwapongeza kwa msaada waliotoa
wanakikundi hao ambapo aliomba kuendelea kutoa misaada kulingana na jinsi
watakavyokuwa wamewiwa ili kuokoa uhai wa watu. Mkenda
aliongeza kuwa Sanitizer walizopokea watagawa kwa watumishi wote bila kuwepo
upendeleo na kuwataka wahudumu wa Afya kwendelea kujikinga na Corona huku
wakitoa maelekezo ya kujikinga na ugonjwa huo kama yanavyotolewa na Wizara ya
Afya. Katika
Baraza hilo Diwani kata ya Roche,Nixon Amolo aliomba halmashauri yake kuitendea haki kata
yake ya Roche kwa kuwakamilishia Wananchi wake miundombinu ya Maji pamoja na
Zahanati ya Ng’ope ili wananchi wanufaike na matunda ya Nchi yao. Naye Diwani
kata ya Kitembe,Thomas Patrick Lissa aliomba halmashauri hiyo kuandaa mpango
mathubuti kwa ajili ya makusanyo kutoka Chanzao cha Barrick ili kuongeza
mapato. Lissa
alisema kuwa halmashauri ya Rorya wanayo haki ya kupata asilimia ya makusanyo
ya mapato yah fedha kutoka Mgodi wa Barrick kutokana na kuwa Mgodi huo ipo Mara na pia
wanachangia miundombinu ya Barabara katika kupitisha vifaa vyao kwenda Nyamongo
huku maji ya sumu yanayotajwa kuadhiri Watu na mifugo wanayatumia watu wa Rorya. Katika swala
hilo mkurugenzi wa halmashauri ya Rorya,Charles Chacha aliwataka madiwani kuwa
wavumilivu wakati hatua zingine
zikichukuliwa kupitia mkuu wa mkoa Mara,Adamu Kigoma Malima.