F Mafuriko yaiathiri Indonesia | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mafuriko yaiathiri Indonesia

Watu elfu 81 wameathiriwa na janga la mafuriko nchini Indonesia.

Budi Budiman Wahyu, Mkurugenzi wa Operesheni wa Shirika la Kupunguza Maafa la Java magharibi, amesema kuwa mvua kubwa ambazo zimekuwa zikinyesha katika mkoa wa Bandung tangu jana usiku zimesababisha mafuriko katika wilaya 5.

Akisisitiza kwamba watu elfu 81 wameathiriwa vibaya na mafuriko katika mkoa huo, Wahyu amesema kwamba takriban watu elfu 2 ambao nyumba zao ziliharibiwa wamehamishwa.

Kulingana na taarifa hiyo,majengo 22,057, ambapo 169 ni majengo ya umma,yameharibiwa na maji ya mafuriko.