Wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha nguo cha Mazava Mkoani Morogoro wamezuiwa kuingia ndani ya kiwanda na kufanya shughuli za uzalishaji wa kiwanda hicho mara baada ya mmiliki wa kiwanda hicho kuwapa likizo ya miezi mitatu bila mishahara ya mwisho wa mwezi mara baada ya kiwanda hicho kukosa oda za uzalishaji kutoka nje ya nchi.
Hata hivyo wafanyakazi wa kiwanda hicho walitangaziwa kupewa posho ya 50% ya mishahara na mmiliki wa kiwanda hicho jambo ambalo wao hawakubaliani nalo wakisema ni kinyume na makubaliano ya mikataba yao.
Hadi sasa bado wafanyakazi Kazi wa kiwanda hicho bado wako nje ya kiwanda hicho wakihitaji kuzungumza na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo.