Na Rebeca Duwe, Tanga
WILAYA Tatu za mkoa wa Tanga zimepatiwa vifaa vya kujikinga na covid 19 zikiwemo ndoo 85 , wilaya hizo ni Tanga jiji , Muheza na Pangani ambapo vifaa hivyo vitagawanywa nakuwekwa kwenye maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu .
Ndoo hizo 85 zenye koki zitawawezesha watu kunawa mikono yao mara kwa mara kwa kutumia maji tiririka kwenye maeneo ya masoko, vituo vya stendi za mabasi na hospitalini katika Wilaya hizo.
Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga Geofrey Hilly alisema vifaa hivyo ni sehemu ya kusaidia juhudi za Serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID - 19 Mkoani Tanga.
Alisema kuwa baadhi ya maeneo ambayo ndoo hizo zitawekwa katika jiji la Tanga ni vituo vya afya Duga ,Ngamiani, Mikanjuni , Pongwe pamoja Masako ya Mgandini, Mlango wa Chuma, Deep sea, na Sahare Kasera .
Akipokea msaada huo wa ndoo mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela Aliishukuru Tanga 'UWASA' kwakutoa ndoo hizo nakuagiza kutumika kama ilivyokusudiwa
" Naomba vifaa hivi visiwekwe stoo Bali vipelekwe kwenye maeneo husika vikafanye kazi ilivyokusudiwa " Alisema Shigela
Shigela Alisema kwa sasa mapambano yaliyopo nikwaajili ya magonjwa yote ya mlipuko " Kwa sasa hivi hatupambani na Corona pekee Bali magonjwa yote ya mlipuko hivyo usafi wa kunawa mikono utakuwa ni utamaduni wetu endelevu , hivyo naomba wilaya zote zihakikishe vifaa hivi vinapatikana maeneo yote yenye mikusanyiko ya watu wengi" Alisema Shigela