Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo limekabidhi shule ya Sekondari ya Wasichana iliyojengwa Kikombo Jijini Dodoma kwa serikali kwa ajili ya kuanza kutumika kwa wanafunzi wa kidato Cha tano na sita kwa mchepuo wa Sayansi.
Ujenzi wa Shule hiyo ni matokeo ya wazo la umoja wa wabunge Wanawake Tanzania katika kuboresha mazingira mazuri kwa mtoto wa kike hapa Tanzania na hatimae kuanza Ujenzi wa Shule hiyo.
Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi wakati wa makabidhiano kati ya Bunge na Serikali kwa ajili ya kuanza kutumika Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, amewapongeza wabunge kwa wazo hilo zuri ambalo linakwenda kuweka alama ambayo haitafutika daima.
"Hakuna Bunge lolote hapa Afrika ambalo limeweza kufanya hivi hicho ni kielelezo tosha kabisa katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha elimu hapa nchini" amesema Mhe. Majaliwa.
Amesema Shule hiyo itaitwa Bunge Girls High School, na itakuwa inachukua wanafunzi kutoka kote nchini Tanzania bara na visiwani.
Aidha ameipongeza Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa kuchangia milioni mia mbili(200) katika kuongeza mchango katika kuboresha elimu hiyo na Serikali itaendelea kuunga mkono sambamba na kuboresha mazingira kwa mtoto wa kike awapo shuleni.
Aidha ameitaka TAMISEMI pindi wanapowapangia wanafunzi katika shule hiyo wahakikishe hata watoto wenye vipaji kutoka vijijini nao wanapewa vipaumbele katika shule hiyo.
Aidha ameitaka kuhakikisha wanadhibiti utoro na Mimba kwa watoto pindi wawapo shuleni na kuchukua hatua kali kwa wale wote ambao wanakuwa wanakwamisha watoto wa kike kupata elimu bora na kusisitiza watoto wa kike kuuchwa wasome bila bugudha.
"Niwatake Wakuu wa Wilaya kote nchini waende wakasimamie Sheria hiyo na kuhakikisha wale wote ambao wanawapa mimba au kuoa wanafunzi wanachikuliwa hatua kali" amesema.
Kwa upande wake Spika wa Bunge Mhe.Job Ndugai amesema Shule hiyo imejengwa kwa mda mfupi Sana kwani Ujenzi wake umeanza mwezi wa kwanza mwaka huu 2020 na mpaka Sasa imeshakamilika na itaanza kutumika Sasa.
Nae Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wabunge Tanzania, Mhe Magreth Sitta amesema umoja huo ulianzishwa mwaka 1993 na ukiwa na wabunge Wanawake ishirini na tatu tu na lengo ni kujenga usawa wa kijinsia kwa jamii.
Amesema hapo awali kulikuwa na matatizo mengi yanayowakumba watoto wa kike na katika kutafuta suruhisho ya jambo hili ndio wakaja na wazo la ujenzi wa Shule hiyo na kubainisha kuwa mpaka Sasa wameshatumia kiasi cha shilingi bilioni 1.4 na itakuwa na michepuo ya PCM, PCB, EGM na PGM.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. amelipongeza bunge kwa ujenzi wa shule hiyo na kwamba itaenda kuboresha elimu hapa nchini na shule hiyo itakuwa ni yamchepuo wa Sayansi ikiwa ni kuimarisha masomo ya sayansi.