F Chifu Adam wa Pili asimikwa rasmi kuwa Chifu wa wahehe | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Chifu Adam wa Pili asimikwa rasmi kuwa Chifu wa wahehe

Chief Adam wa Pili Adam Abdul Adam Sapi Mkwawa Mwamuyinga jana alisimikwa rasmi na kukabidhiwa miiko ya utawala wa kabila la Kihehe baada ya kufikisha umri wa kuongoza.

Hafla hiyo imefanyika katika Uwanjani wa Mashujaa uliopo Kalenga Mkoani Iringa ambapo Umoja Wa Machief Tanzania UMT umeshiriki.

Chief Adam wa Pili anachukua nafasi ya baba yake, Chief Abdul Mfwimwi aliyefariki mwaka 2015 February 14.