Kambi ya mafunzo ya jeshi la Somalia inayoratibiwa na Uturuki yaponea chupuchupu kushambuliwa.
Taarifa zilizotolewa kuhusu Somalia zimefahamisha kwamba kambi ya mafunzo ya jeshi la Somalia na Uturuki imeponea chupuchupu kushambuliwa na mtu aliekuwa akitaka kujitoa muhanga n dhidi ya kambi hiyo.
Balozi wa Uturuki mjini mogadishu Mehmet Yılmaz amesema kwamba gaidi aliekuwa amejipeneyeza katika kundi la wanafunz waliokuwa katika kambi hiyo wakati wa uchaguzi katika kambi ya TURKSOM aligunduliwa na wanajeshi waliokuwa katika doria na kumuangamiza papo hapo.
KUlingana na taarifa za awali kuhusu tukio hilo, mtu huyo alikuwa akijaribu kujipenyeza katika eneo ambalo kunapatikana wanajeshi wa Somalia licha ya kutadharishwa na kuombwa arudi nyuma alionekana kuendelea kusonga mbele na kupelekea kufyatuliwa risasi.
Raia mmoja pia ameuawa katika shambulizi hilo.
Jeshi la Uturuki linatoa mafunzo kwa jesh la Somalia kwa ajili ya kuimarisha usalama katika taifa lao na kukabiliana na wanagambo ambao mara kwa mara husababisha kuyumba kwa usalama na kuendeshwa kwa mashambuliz ya kujitoa muhanga.
Katika miaka michache ya nyuma, Uturuki imeimarisha ushirikiano wake na Somalia katika sekta tofauti ikiwemo ulinzi na uchumi.