F Madiwani halmashauri ya Rorya wamtwisha mzigo mkuu wa mkoa Mara | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Madiwani halmashauri ya Rorya wamtwisha mzigo mkuu wa mkoa Mara



Na Timothy Itembe Mara.

MADIWANI wa halmashauri ya Rorya mkoani Mara jana katika kikao cha Baraza la Hoja za mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG wameeleza changamoto mbalimbali za maendeleo ambazo zinakabili  kata wanazotoka.

Changamoto moja wapo ni pamoja na kero ya kukosa mawasiliano ya mitandao ya Simu huku wakazi wengi wengi wa Rorya  wakilazimika kununua na kutumia lainiza za Simu ikiwemo mitandao simu ya kutoka  Nchi jirani ya Kenya ili kurahisisaha mawasiliano.

Akiongea mbele ya mwenyekiti wa kikao hicho   ambaye pia ni mkuu wa mkoa Mara,Adamu Kigoma Malima Diwani kata ya Kitembe,Thomas Patrick Rissa alisema kuwa baadhi ya kata ndani ya halmashauri ya Rorya ikiwemo kata ya Kitembe wananachi wake wanateseka kwa kukoswa mawasiliano ya simu huku wengiwake wakilazimika kununua na kutumia laini na mitandao ya simu kutoka Nchijirani ya Kenya.

“Mheshimiwa  mkuu nwa mkoa Mara tunaomba utusaidia swala kubwa la kukoswa mawasiliano ya simu watu wa Rorya ambapo mawasiliano ni shida kutokana na mitandao ya simu za Tanzania kuzidiwa na mitandao ya simu kutoka Nchi jirani ya Kenya jambo ambalo linasababisha wakazi wengi wa Rorya kununua na kutumia laini na mitandao ya simu kutoka Kenya”alisema Rissa.

Kwa upande wake Roja Okuku alisema kuwa Tarafa ya Nyancha haina shule ya kidato cha Tano na sita licha ya kuwa Tarafa hiyo inawapiga kura wengi ikilinganishwa na Tarafa zingine za Rorya.

Okuku aliongeza kuwa Wanafunzi wa Tarafa ya Nyancha wanateseka kwa kutembea mwendo mrefu huku wakifuata masomo ndani ya Tarafa zingine jambo ambalo linachangia kuwepo na mimba mashuleni.

Mkuu wa mkoa Adamu Kigoma Malima alisema kuwa kero hizo ataendelea kukabiliana nazo kwasbabu yeye ni mwenyekiti wa mkoa Mara na ndiye mkuu wa mkoa huo kwa hali hiyo wakati wanaenda kipindi cha kuvunja Baraza na kuelekea uchaguzi mkuu 2020 Okotoba atahakikisha anazungumza na wahusika ili kutatua changamoto hizo na wananchi wakaendelea kunufaika na matunda ya Nchi yao.