Mwili wa marehemu mke wa Meneja wa WCB, Babu Tale, Shamsa Kombo 'Shammy' aliyefariki dunia asubuhi ya jana katika Hospitali ya Muhimbili unatarajiwa kwenda kuihifadhiwa mjini Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wanafamilia wa marehemu.
Marehemu enzi za uhai wake alifahamika zaidi kutokana na asasi yake aliyoimiliki ya "Nasimama Nao" iliyokuwa ikiwasaidia kina mama na mpaka mauti yalipomkuta ameacha watoto watatu, wawili wa kiume na mmoja wa kike.