Ujerumani yaondoa tahadhari za usafiri kwa mataifa mengi ya Ulaya


Ujerumani imeondoa tahadhari za usafiri kimataifa ilizoweka kwa mataifa mengi ya Ulaya miezi mitatu iliyopita kutokana na mripuko wa virusi vya corona.

Wizara ya Mambo ya nchi za nje ya Ujerumani, imeondoa masharti hayo ya usafiri kwa mataifa 27 ya Ulaya kuanzia usiku wa kuamkia leo.

Ujerumani pia inatarajiwa kusitisha vizuizi vyake katika mipaka yake kuanzia leo. Hatua hiyo inaenda sambamba na pendekezo la kamisheni ya Umoja wa Ulaya linalozimihimza nchi wanachama kufungua mipaka kuanzia wiki hii.

Hata hivyo raia wa Ujerumani bado wanashauriwa kuepukana na safari ambazo si za lazima nje ya nchi ambazo tahadhari hazijaondolewa.