F Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza afariki dunia | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza afariki dunia

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amefariki dunia kutokana na shambulio la moyo, kwa mujibu wa taarifa ya serikali. Nkurunziza ambaye alikuwa anamaliza muda wake wa urais amefariki katika hospitali ya Karusi alipokuwa amelazwa jana.

Kulingana na msemaji wa serikali, balozi Willy Nyamitwe, Rais Pierre Nkurunziza amefariki kwa mshtuko wa moyo kinyume na uvumi unaoenezwa.

Serikali ya Burundi imetangaza siku saba za maombolezi na anatuma risala za ramirambi kwa familia.

Rais Pierre Nkurunziza alizaliwa Desemba 18, 1963 mwansiasa wa Burundi ambaye amekuwa madarakani tangu 2005.

Alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha CNDD-FDD, hadi alipochaguliwa kama rais wa Burundi.

2015, Nkurunziza alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa na utata na chama chake kwa muhula wa tatu ofisini.

Wafuasi wake na wanaompinga Nkurunziza walikosa kukubaliana katika suala la ikiwa ilikuwa halali kwake kugombea tena na maandamano yakafuata.

Zaidi ya miezi miwili kulitokea maandamano ya kumpinga Nkurunziza ambayo yaliandamana na ghasia na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 100.

Mei 13, 2015, jaribio la mapinduzi dhidi ya Nkurunziza lilitokea akiwa nje ya nchi hiyo.

Mkuu wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare alidai kwamba amemng'oa mamlakani Nkurunziza lakini wanajeshi watiifu kwa Nkurunziza walikanusha madai hayo.