DURU la Uchukuaji wa Fomu ya Kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, laendelea kupamba moto ambapo aliekuwa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar Rashid Ali Juma amaejitokeza ofisini hapo kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho.
Rashid Ali Juma pia alikuwa Waziri wa Habari,Utamaduni na Utalii Zanzibar na Mwakilishi wa Jimbo la Amani Unguja.
Mara baada ya Zoezi la Uchukuaji wa Fomu aliwaambia Waandishi wa Hbari kwamba leo sio siku ya kuzungumza mengi kitendo kilicho mleta ni uchukuaji wa fomu tu, hivyo wacha aende kuzisoma na kujua kilicho andikwa ndani ya fomu hizo.
“Napenda kuwashukuru ndugu zangu waandishi wa Habari kwa kazi kubwa munayoifanya, kikubwa leo kilichonileta hapa ni tukio kubwa la kihistoria kwangu kuchukua fomu na nimeshafanya hivyo niwaombe nikasome ili kujua kilichoandikwa humu ndani” alisema Rashid Ali Juma.
Rashid Ali Juma anakuwa mgombea wa 16 kujitokeza katika ofisi kuu za chama hicho kisiwandui Mjini Unguja na kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia chama cha Mapinduzi CCM.