F Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini atangaza nia ya kugombea urais na ataja vipaumbele vyake. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini atangaza nia ya kugombea urais na ataja vipaumbele vyake.



Duru kumtafuta Mgombea wa Nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia Makini lafunguliwa ambapo Katibu Mkuu wa chama hicho  Ameir Hassani Ameir ametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo na ameahidi endapo wananchi watamchagua  kuboresha Sekta ya Elimu na Sekta ya Afya.


Akizungumza na Mwandishi wetu mara baada ya kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo, Ameir alisema kwamba endapo Chama chake cha Demokrasia Makini kinampa nafasi ya kukiwakilisha katika Uchaguzi Mkuu  kwa kugombea nafasi ya nafasi ya Urais wa Zanzibar na kupata ridha kwa wananachi anaahidi kuwaletea maendeleo makubwa katika Sekta ya Elimu na Technolojia pamoja na Sekta ya Afya.

Ameir alisema kwamba vipaumbele vyake endapo  atachaguliwa kuwa mgombea wa nafasi hiyo na Kupewa ridhaa kwa Wananchi ni kuboresha kwa kasi Sekta ya Elimu nchini ambapo alisema bado haijafikiwa ipasavyo.

“Vipaumbele vyangu ni vingi sana lakini endapo ntachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar naahidi kuboresha Elimu hasa Sayansi na technolojia pamoja na asfya bure kwa Wanzanzibar wote” alisema Ameir Hassan Ameir.


Pia Katibu Mkuu huyo Ameir Hassan Ameir alisema atadumisha Huduma zote muhimu kwa Wananchi kama vile maji safi na salama  na kusema kuwa huduma zote zitakuwa ni bure.

Aidha alisema kuwa atahakikisha anakuza Utalii wa Zanzibar wenye  tija kwa wananchi wote ambapo atazalisha ajira nyingi kwa vijana na kukuza pato la taifa na pato la mtu mmoja mmoja kupitia Sekta hiyo.

“Endapo ntachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar huduma muhimu kama vile maji safi na salama itakuwa bure lakini ntahakikisha Utalii uliokuwa katika visiwa hivi unawanufaisha wanzanzibar wenyewe kwa kuzalisha ajira nyingi sana” alisema Ameir Hassan Ameir.

Katika Maelezo yake Katibu Mkuu huyo alisema  pia atahakiksha Zanzibar inajengeka kimiundombinu ilikuwa mzuri ambapo atashadihisha kujengwa kwa viwanda vikubwa na vidogo kwa lengo la kuongeza uzalishaji pamoja na kuzalisha ajira kwa vijana visiwani humo.

Hadi sasa Jumla ya wagombea wawili tayari wameshatangaz nia ya kugombea nafasi hiyo ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho cha Demokrasia Makini.