"Hayati Benjamin Mkapa alianza kazi Serikalini kama Afisa Tawala wa Wilaya ya Dodoma Aprili 1962, baada ya miezi minne alijiunga na masomo ya Shahada ya Uzamili nchini Marekani na aliporudi alifanya kazi katika Wizara ya Mambo ya Nje" -Profesa Kabudi
"Hayati Benjamin William Mkapa, alifariki kwa ugonjwa wa Moyo kusimama ghafla, ulioandamana na Malaria, Julai 23, 2020, majira ya saa 3:30 usiku akiwa na umri wa miaka 81" -Profesa Kabudi