Na Faruku Ngonyani, Mtwara
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya ametoa siku 30 kwa mamlaka inayoshughulikia barabara za mijini na vijijini (TARURA) kuahakikisha wanachonga barabara zote zilizopo mtaa wa Tandika Halmashauri ya Manispaa Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara.
Ametoa agizo mara baada ya kupokea kero za ubovu wa barabara hizo za mitaa kutoka kwa wananchi wa mitaa hiyo mara baada kufanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi hao.
Huo ukiwa ni mwendelezo wa Mkuu huyo wa Wilaya wa kusikiliza kero za wananchi wa Wilaya ya Mtwara ambapo mpaka sasa kero kubwa zilizpo ndani ya Wilaya hiyo ni pamoja na kero za Ardhi,barabara pamoja kero ya maji kwa baadhi ya maeneo.
Wananchi hao wamesema kuwa kwa sasa barabara hiza za mitaa haziwezi kupitika kwa gari hali inayohatarisha maisha yao kwani muda mwingine wanapata changamoto juu wagonjwa haswa akina mama wajawazito pindi wanapokuwa tayari kwenda hospatalini kwa kujifungua.
Aidha wananchi hao wamekuwa na hali ya kushangazwa pindi walipoambiwa na Tarura kuwa barabara zinazotambulika kwenye mpango zipo tatu huku Halmshauri wanatambua kuwa barabara zote zipo kwenye mpango.
“tunashangaa kuona tarura wanasema kwamba barabara zilizopo kwenye mpango tatu wakati kabla hawa Tarura hawajaja Halmashsuri walikuwa wanazimbua hizi baraba”.