Mwenyekiti Halmashauri Bagamoyo atetea Kata yake



Na Omary Mngindo, Fukayosi.


MWENYEKITI aliyemaliza muda wake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Ally Ally, jana amepeta kwenye kura za maoni nafasi ya Udiwani wa Kata ya Fukayosi.

Katika kura za maoni zilizofanyika shule ya Msingi Fukayosi na kuhudhuliwa na wapigakura 112 kati ya 116, chini ya Msimamizi Elia Macha akisaidiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata hiyo Olnjurie Marigwa, Ally alipata kura 96, dhidi ya wagombea wenzake Fadhili Sembeke 1 na Msunye Selemani 7.

Kwenye zoezi hilo ambalo jumla kuu ya wapigakura ilitakiwa iwe 116, kati ya hao wanne hawakuweza kuhudburia, hatua iliyomfurahisha Marigwa ambapo aliwatangazaia wajumbe na waarikwa kwamba mkutano huo ni halali, huku akiwaomba wajumbe kuhakiki majina kabla ya kuanza kwa zoezi hilo.

 "Nataka mkutano wetu uwe wa kisasa zaidi, hivyo wajumbe wote tujiridhishe majina yetu kwa utaratibu wa kuita majina kulingana na matawi yetu yanayounda Kata kichama, dhamira yake ni kumpata mgombea pasipokuwa na malalamiko," alisema Marigwa.

Baada ya mwongozo huo utaratibu wa upigaji kur ukafanyika kwa wenyeviti kuongoza mistari wakimalizia Makatibu, zoezi lililokuwa la kisasa zaidi kabla ya Macha kukabidhiwa jukumu la kutangaza matokeo ikiashiria kumalizika kwa zoezi hilo, ambapo alitangaza maajina ya wagombea watatu na kura walizozipata.

"Kwa mamlaka niliyopewa ya kusimamia zoezi hili, nitumie muda huu kutangaza matokeo baada ya kukamilika kwa hatua ya upigaji wa kura wa kumpata mgombea wetu wa Udiwani nadni ya Kata ya Fukayosi, litalokwenda ngazi za juu kisha kutuletea jina watalilipendekeza kwa hatua zingine," alisema Macha.

Marigwa amizungumza na Waandishi wa habari alisema kuwa zoezi limekwenda kwa amani na Uhuru mkubwa, huku akitumia fursa hiyo kuwaasa wana-CCM katani halo kwa hakuna sherehe, wala lulashifiana kwani ndani ya chama hicho hakuna mshindi.

Kwa upande wao wagombea hao walielezea zoezi hilo, huku Ally akiwashukuru wajumbe kwa kuonesha imani nao, ambapo alisema anasubiri vikao vya juu vya maamuzi, jina lake likirudi na kutetea nafasi hiyo atamalizia kazi iliyosalia.

Nao Sembeke na Seleman walielezea mchakato ulivyokwenda, huku wakiwashuru wajumbe kwa kutimiza haki zao za kuchagua viongozi kwenye nafasi hiyo.