Mhe. Rais Magufuli leo tarehe 10 Julai, 2020 amemteua Bw. Gabriel Pascal Malata kuwa Wakili Mkuu wa Serikali akichukua nafasi ya Dkt. Julius Clement Mashamba.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Boniface Luhende kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali akichukua nafasi ya Bw. Gabriel Pascal Malata.
Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 10 Julai, 2020.