F UAE yazindua safari ya kwanza kwenda sayari ya Mars | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

UAE yazindua safari ya kwanza kwenda sayari ya Mars


Umoja wa Falme za Kiarabu imeweka historia kwa kutuma chombo chake katika sayari ya Mihiri yaani Mars baada ya kufanikiwa kukirusha kutokea nchini Japani.

Chombo chake cha Hope kimerushwa kwa roketi ya H2-A kutoka kituo cha anga za juu cha Tanegashima na huenda sasa hivi kimeshapita kilomita milioni 500 kikielekea kufanya utafiti kuhusu hali ya hewa na anga katika sayari ya Mahiri.

Majaribio mawili ya awali ya kurusha chombo hicho wiki jana yalilazimika kufutwa kwasababu ya hali mbaya ya hewa.

Kuwasili kwa chombo Hope Februari 2021 kumepangiwa kusadifiana na maadhimisho ya miaka 50 tangu kuundwa kwa Muungano wa Falme za Kiarabu.

Mheshimiwa Bi. Sarah Al Amiri, anayeongoza kikosi cha chombo Hope, alizungumzia faraja yake na furaha aliyonayo kuona chombo hicho kikipaa salama kwenye anga. Na kusema kwamba hali itakayoshuhudiwa nchini kwao Julai 20, ni sawa tu na Marekani wakati raia wake waliposhuhudia chombo Apollo 11 Moon kikitua miaka 51 iliyopita,

"Ilikuwa kichocheo kwa kizazi chote kilichotazama ikipaa na kuwa na ndoto kubwa zaidi," ameiambia BBC News.

"Leo hii ninafuraha sana kwamba watoto wa Emirates asubuhi ya Julai 20, wakiwa na mradi wao unaoendelea, wakijionea uhalisia mpya wa mambo, uwezekano mpya ulio wingi wa matumaini, unaowaruhusu kuchangia zaidi na kuwa na mchango mkubwa duniani."

Chombo cha UAE ni moja na vyombo vitatu vilivyokwenda kwenye sayari ya Mahiri mwezi huu.

Marekani na China zote zina ujumbe wao unaotaka kwenda kwenye sayari hiyo ambao uko katika hatua za mwisho za matayarisho.

Ujumbe wa Marekani unaotumia chombo kwa jina Perseverance, umetuma pongezi zao kwa Hope. "Nasubiri kwa hamu kuunga na nyinyi kwenye safari hii!" umeandika kupitia akaunti yao ya Twitter.