F Urusi yatangaza meli za kivita zenye silaha za kisasa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Urusi yatangaza meli za kivita zenye silaha za kisasa

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza kuwa meli za kivita za Urusi zitawekwa silaha za kisasa, za kasi na zenye utendaji mkubwa zaidi.Katika gwaride la jeshi la wanamaji leo Jumapili, Putin amesema jeshi hilo litakuwa la kipekee kutokana na teknolojia ya hali ya juu na silaha za kisasa.

Putin ameongeza kuwa silaha hizo za kisasa zitakuwa moja ya njia bora za kujilinda.Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la TASS, wizara ya ulinzi pia ilitangaza mafanikio katika majaribio yake ya kombora la kasi la Zircon.

Jeshi la wanamaji pia lilisheherekea kwa kuandaa magwaride katika miji mengine ya Pwani ya Urusi.Katika video iliyotolewa na wizara ya ulinzani, Urusi ilizionyesha meli zake za kivita, manowari pamoja na helikopta na ndege za mwendo kasi.