Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za Mitaa Tamisemi,Mwita Mwikwabe Waitara amechukua Fomu za kugombea Ubunge ndani ya Jimbo la Tarime Vijijini ili kumung'oa John Heche.
Mwita Waitara alitaja sababu zinazo msukuma kwenda kugombea jimbo la Tarime na kuacha jimbo la Ukonga Jijini Dar es Salaam na kutaka kugombea Tarime kwa sababu ni Nyumbani alipozaliwa na kuwa hiyo ni adhima yake tangu hapo nyuma.