F Yajue mahitaji makuu ya mafanikio kwa msaka mafanikio | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Yajue mahitaji makuu ya mafanikio kwa msaka mafanikio

Mahitaji makuu ya mwandamu katika kuishi vyema hapa duniani anahitaji chakula, mavazi na maradhi, hii ni kwa mujibu ya mwalimu wangu ambaye aliwahi nifundisha miaka ya nyuma kidogo. Lakini tukiachana na mahitaji hayo, Itakuwa ni vigumu sana kama unataka kufikia ndoto yako kama hautakuwa na vitu vifuatavyo.

1. Lengo kuu.
Lengo kuu hutokana na malengo mengine madogo madogo. Kama ilivyo, ili iitwe bahari ni lazima bahari hiyo iweze kupokea maji kutoka vyanzo vingine vya maji kama vile vijito, mito, mabwawa na mengineyo ndipo itatokea bahari. Kwa kuona mfano huo tunaweza tuangalie mfano mwingine ambao itatusaidia kufukia lengo kuu,

kama unahitaji kuwa mfanyabiashara mkubwa unahitaji kuwa na malengo mengine madogo madogo ambayo ndiyo yatakufanya kukamilika kwa lengo hilo kuu. Hivyo kila wakati ikumbukwe ya kwamba ni lazima uweze kuyapapalilia vyema malengo yako madogomadogo kwani ndiyo chanzo kikubwa cha kufikia mafanikio yako.

Hivyo ili uweze kuwa mwenye mafanikio makubwa kwa upande wako unahitaji kuwa na lengo kuu ambalo litakufanya uwezo kutimiza ndoto yako.

2. Sababu
Hakuna mafanikio bila ya kuwa na sababu ya kufanya kitu hicho. Kila kitu inachokiona katika dunia hii kumbuka ya kwamba mwanzilishi wa kitu au jambo hilo alilianzisha kwa sababu maluumu. Huwezi kusema unataka kufanya jambo fulani kama huna sababu, kwani mafanikio ya aina hiyo utawasikia kwa majirani tu.

Hivyo kila wakati kwa kila jambo ambalo unalitaka kulifanya, kabla ya kufanya jambo hilo kumbuka ya kwamba ni lazima utafute sababu ya kufanya jambo hilo. Kama hautapata majibu ya kufanya jambo hilo ni vyema akaliacha kulifanya, kwani kama utaamua kulifanya jambo bila ya kuwa sababu, jambo hilo litakufa tu baada ya siku chache. Hivyo kumbuka kila kitu ambacho unakifanya au unataka kukifanya ni lazima kuwe na sababu maalumu.

3. Msukumo wa kiutendaji.
Mafanikio hayajatokea kama ajali kama hakutakuwa na msukumo wa kiutendaji juu ya jambo hilo. Msukumo humfanya Mtendaji wa jambo hilo kuweza kutendeka kwa ufasaha kila wakati. Hivyo kila wakati usifanye kitu kwa sababu mtu fulani amesema ufanye, kwani kama atafanya hivyo utakosa hamasa ya msukumo juu ya utendaji wa jambo fulani.

Hivyo kuwepo kwa lengo kuu, sababu ya kutenda jambo na msukumo wa kiutendaji hiyo ndiyo siri kubwa iliyojificha katika kufikia ndoto ambayo unayo.

Na. Benson Chonya