F Zuchu Apewa Zawadi ya gari na diamond,Amwaga machozi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Zuchu Apewa Zawadi ya gari na diamond,Amwaga machozi


Staa wa muziki nchini, diamondplatnumz amemzawadi Zuchu gari mpya aina ya Toyota Vanguard hapo jana katika show ya Big Sunday Live ya Wasafi TV.

Zawadi hiyo imetolewa ndani ya saa 24 tangu #Zuchu afanye show kubwa yenye mafanikio makubwa ndani ukumbi wa Mlimani City ya kuwashukuru mashabiki zake kwa mapokezi makubwa waliyompatia kwa kipindi kifupi alichokuwepo kwenye muziki.

Ikumbukwe kuwa, Malkia huyo mpya wa kizazi kipya, officialzuchu amezawadia gari ikiwa ni miezi mitatu tu tangu ajiunge na lebo ya WCB ambayo inamilikiwa na Diamond.