F Faida zitokanazo na ulaji wa ugali wa dona | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Faida zitokanazo na ulaji wa ugali wa dona


Watu wengi hupendelea ugali mweupe, au watu wengine hupenda kuuita sembe, Faida ya sembe ni vile unavyoweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu bila kuharibika kuliko dona na wapo wengine huipenda sembe labda inavutia machoni tu kutokana na rangi yake.

Ila ulaji wa dona na dona la mahindi ya njano una faida nyingi kiafya na kiuchumi!

1. Una virurutbisho muhimu vikiwemo vitamini na madini mbalimbali yanayohitajika kwa afya ya mwili na akili. Katika sembe virutubisho vyote huondokewa kwa kukoboa.

2. Una nyuzi lishe ambazo husaidia msukumo na mmeng'enyi wa chakula, hivyo huzuia matatizo ya kukosa kubwa na hata saratani ya utumbo mpana.

3. Hupunguza hatari ya kupata magonjwa yasiyiambukizwa yakiwemo kisukari, uzito kupita kiasi, shinikizo la damu n.k kwa sababu kiasi cha wanga kinachoweza kuchukuliwa huwa kidogo kwenye dona kuliko sembe.

4. Mahindi ya njano yana vitamin A kwa wingi ambayo ni muhimu kwa afya ya macho, ngozi na mifumo mbalimbali mwilini.

5. Unapunguza gharama na muda wa kukoboa na kutupa chakula kama mapumba.

Wengi tunashangaa mbona kasi ya magonjwa ni mengi kuliko zamani kumbe wachawi ni sisi wenyewe. Hebu anza leo kula ugali wa dona uone maajabu yaliyo ndani yake.