Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Arusha ,wamekamata dawa za kulevya aina ya bange magunia 116 ,pamoja na watuhumiwa 3 katika kitongoji cha Karatini Kisimiri chini wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha katika operesheni ya biashara haramu ya bangi .
Katika operesheni iliyoongozwa na Kamisha Jeneral Wirbert Kaji pamoja na Kamanda wa polisi mkoa wa rusha ACP Salum Rashid Hamdun, pamoja na magunia 116 vilikamatwa viroba tisa(9)vya bangi na misokoto 714 ya bangi.
Mtuhumiwa mmoja Kanael Ndakausi (50)Akyoo mkazi wa Karatini Kismiri chini alikamatwa akiwa nagunia (3) za bangi na viroba ( 9)vya bangi vyote vikiwa vimehifadhiwa ndani ya nyumba yake
Aidha magunia mengine 113 yalikamatwa kwenye nyumba zaidi ya 20 za wakazi wa eneo hilo ambapo watuhumiwa walifanikiwa kukimbia makazi yao kabla ya kukamatwa,ambapo mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamishana Jenerali James Wirbert Kaji alisema baadhi ya watuhumiwa wamekimbia hivyo dawa hizo za kulevya ambazo hazikuwa na watuhumiwa wameziteketeza
Aidha Kamisha Kaji alitoa onyo kali huku akisema kuwa Arumeru imekuwa ni tatizo kubwa kwani hivi karibuni waliweza kukamata zaidi ya gunia 140 ambapo wamekamata gunia 116,amewasihi wananchi kwa Tanzania nzima wazidi kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwani bangi siyo nzuri na vita hiyo ni vita ya wotena siyo ya mamlaka peke yake .
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Arusha (ACP)Salum Hamdun amesema Jeshi litaendelea kufanya operesheni katika kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi vya ulinzi na usalama, amesema hata kukamatwa kwa magunia hayo 116 ni matokeo ya ushirikiano baina ya Jeshi la polisi,Mamlaka ya Udhibiti na vyombo vingine vya usalama
Amesema hapo siyo mwisho wataendelea kufanya oparesheni za mara kwa mara japo kuwa bangi hiyo hulimwa milimani na wakati mwingine inakuwa ni vigumu kufika huko lakini jeshi hilo litajitahidi kuhakikisha kwamba kilimo hicho cha bangi kinadhibitiwa .
Ametoa rai kwa watendaji wa serikali katika ngazi vitongoji,vijiji kutokukaa kimya pale wanapoona viashiria hivyo na kuwataka kutoa taarifa za mapema kwa kushirikiana na wananchi raia wema, ili kuhakikikisha kwamba kilimo hicho cha bangi kinakoma.
0 Comments