F Kikosi cha simba kutua leo Dar | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kikosi cha simba kutua leo Dar


BAADA ya Kikosi  cha Simba jana kutwaa ubingwa  wa Kombe la Shirikisho kilirejeai jijini Mbeya.

Leo saa 2:20 asubuhi kitaondoka kwa ndege kurudi jijini Dar es Salaam.

Simba ilishinda mbele ya Namungo FC kwa ushindi wa.mabao 2-1 mchezo wa fainali iliyochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.

Mabao ya Simba jana, Agosti 2 yalifungwa na Luis Miqussone na John Bocco huku lile Namungo FC likifungwa na Edward Manyama.

Sven Vandenbroeck,  Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wamepambana kufikia mafanikio jambo lililowapa ushindi.

"Wachezaji wamepambana kwa kadri ya uwezo wao jambo lilitupa ushindi,  wapinzani wetu wameonyesha ushindani pia," amesema.