Na Faruku Ngonyani , Mtwara
Ikiwa leo Ni siku ya urejeshwaji wa Fomu za wagombea nafasi mbalimbali hapa nchini ya kuomba ridhaa ya nafasi za uongozi mamia ya wananchi Jimbo la Nanyamba Mkaoni Mtwara wamejitokeza kumsindikiza Chikota juu ya urejeshwaji wa fomu ya kugombea Ubunge (Ccm) katika Jimbo hilo.
Fomu hiyo imekabidhiwa kwa msimanzi wa Uchaguzi Jimbo la Nanyamba ambaye pia Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nanyamba ndg Thomas Edwin Mwailafu .
Ureshwaji wa fomu kwa wagombea wote hapa Nchini Ni ishara ya kunza kwa kampeni za kuomba kura kwa wananchi ili waweze kuchaguliwa kuwa viongozi kwa miaka mitano (5).
Ikumbukwe uchaguzi Mkuu hapa Nchini unataji kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020 ambapo wananchi watapata fursa ya kuwachagua Madiwani ,Wabunge ,wawakilishi pamoja na nafasi ya Urais
0 Comments