INAELEZWA kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa zamani wa Simba, Senzo Mazingisa, Jumatatu jioni Agosti 10, 2020 alikabidhi ofisi na nyaraka za klabu hiyo.
Kuhusu mbadala wake, ‘kigogo’ mmoja wa klabu hiyo huyo amesema; “Kuna kikao kinaendelea leo ambacho wanajadili nani atakaimu kwa wakati huu huku mchakato mwingine wa kutangaza ajira ukifuata hapo baadaye.”
“Nafasi ya CEO ni ya kuajiriwa hivyo taratibu zote za ajira zinapaswa kufuatwa, ni lazima kutuliza akili kufanya hivyo, lakini mtu wa kukaimu atapatikana na huenda akatangazwa hata leo hiihii,” amesema
Imeelezwa kwamba mtu atakayepatikana kukaimu nafasi hiyo kutoka ndani ya kikao hicho hapaswi kutoka kwenye Bodi ya Wakurugenzi kwa maana kuwa asiwe mjumbe wa bodi hiyo.
Crescentius Magori ambaye alimkabidhi majukumu Senzo ni miongoni mwa wanaotajwa kukaimu kiti hicho.
Senzo alibwaga manyanga ndani ya Simba Agosti 9 kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuwa akiskilizwa huku taarifa nyingine zikidai kwamba mkataba wake ulikuwa umeisha.
0 Comments