Rais wa Uturuki Recep tayyıp Erdoğan azungumza na rais wa Urusi Vladimir Putin kwa njia ya simu kuhusu masuala tofauti katika ushirikiano uliopo kati ya mataifa hayo mawili.
Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili kuhusu hatua ambazo zimekwishapigwa katika ushirikiano kati ya Uturuki na Urusi.
Uturuki na Urusi ni mataifa ambayo yamepiga hatua kubwa katika sekata tofauti ikiwemo katika sekta ya utalii.
Raia kutoka nchini Urusi ni miongoni mwa watalii wengi ambao hutembelea Uturuki katika msimu wa kiangazi.
Uturuki na Urusi ni mataifa mabyo yanashirikiana katika sekta ya uchukuzi , nishati, uchumi na vile vile katika kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.
Taarifa iliotolewa na kitengo kinachohusika na upashaji habari ikulu mjini Ankara zimefahamisha kuwa katika mazungumzo yao rais Putin na ErdoÄŸan wamezungumzia pia hali inayoendelea nchini Libya , ukanda wa Meidterania na mapambano dhidi ya virusi vya corona.
Rais Putin pia amezungumza kuhusu umuhimu wa mazungumzio kuhusu hali inayoendelea katika ukanda wa Mediterania upande wa Mashariki.
Kwa kumalizi mazungumzo yao , rais ErdoÄŸan na rais Putin wanejadili kuhusu Syria na kusema kuwa harakati za kidiplomasia kupatia suluhisho hali inayoendelea nchini Syria kupatiwa suluhisho.
0 Comments