Shirika la mpango wa chakula WFP linaonya kuwa Lebanon huenda ikakosa chakula cha kutosha kwani nchi hiyo ya Mashariki ya Kati huagiza asilimia 85 ya chakula chake kutoka nje.
Msemaji wa shirika la UNICEF Marixie Mercado amesema kuwa kiasi cha nyumba za watoto 80,000 hadi 100,00 zimeharibiwa na sasa watoto hao hawana makao.
Wakati huohuo, WHO imesema imepoteza bidhaa zake kadhaa katika mlipuko huo ikiwemo kontena zilizokuwa na vifaa vya matibabu na vifaa vya kinga dhidi ya Covid-19 vikiungua na kuteketea kabisa.