F Kaya masikini Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kunufaika na TASAF | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kaya masikini Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kunufaika na TASAF


Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Wawezeshaji wa TASAF kupitia Mpango wa kunusuru Kaya Masikini Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara wamekula kiapo Cha uamininifu kabla ya kuanza kwa zoezi la malipo kwa Walengwa.

Zoezi hilo limefanyika katika Ofisi za TASAF na kusimamiwa na Wakili Msomi, Arthur Mbena ambapo Wawezeshaji walimalizia kwa kusaini viapo hivyo.

Nae Mshauri wa TASAF Bi. Maleso Chogo, amewasisitiza Wawezeshaji kuzingatia sheria na taratibu katika malipo kwa Walengwa wa Vijiji vyote 57 vilivyopo kwenye Mpango.

Aidha Bi Chongo aliongeza kuwa taratibu za malipo kwa awamu hii zimeboreshwa huku zikiwataka Walengwa kuja wenyewe kupokea Ruzuku ili kuondoa malalamiko ya dhuluma dhidi ya waliokuwa wanawatuma kuwachukulia hapo awali.

Zoezi la malipo linafanyika Mara baada ya kumalizika kwa Uhakiki wa Kaya maskini uliofanyika mwezi Agosti mwaka huu ambapo watakaolipwa ni wale amabao walifanyiwa Uhakiki huo.

Post a Comment

0 Comments