Translate message
Turn off for: Swahili
Na Timothy Itembe Mara
Wamawake wametoa kilio cha kupata maji safi na salama kwa sababu maji ni muhimu kwa viumbe vyote duniani.
Joyce Ryoba Mang'o mkzai wa Ichugu alisema kuwa bila maji hakuna uhai. Aidha maji ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
"Kiwango cha maendeleo ya jamii yoyote kinategemea kuwepo kwa maji ya kutosha na yenye ubora unaotakiwa. Katika hali yake ya asili, maji ni sehemu ya mazingira ambapo wingi na ubora wake ndio unaosaidia katika kuamua jinsi maji yatakavyotumika. Upatikanaji wa maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na usafi wa mazingira ni muhimu katika kulinda afya za wananchi"aliongeza kusema Mang'o.
Wakina mama hao walitoa kilio hicho mbele ya mgombea ubunge jimbo la Tarime vijijin,Mwita Waitara ambaye pia ni Naibu zari ofisi ya rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi 2020 uliofanyika Kijiji cha Nyamwaga jana.
Pia Mang'o alisema kuwa Utumiaji wa maji ambayo sio salama na uhaba wa maji huchangia katika kusababisha milipuko na kuenea kwa magonjwa kama kuhara na kipindupindu.
Japokuwa maji ni muhimu kwa uhai wa viumbe, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hakuna uwiano wa mgawanyo wa maji ulio sawa kati ya sehemu moja na nyingine na katika majira mbalimbali ya mwaka. Aidha alimaliza kusema Mang'o.
Kwa upande wake Veronika Gabriel kmazi wa Nyamongo alisema kuwa wingi wa maji yanayofaa kwa matumizi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi una kikomo, na maji hayo pia yanaweza kuathirika kirahisi.
Katika kuhakikisha mwanamke anafanya shuguli zake vizuri kuna haja kumpa unafuu mwanamke ambapo serikali inatakiwa itekeleze sera ya maji kote nchini lengo ni kumtua mama ndoo kichwani na kuondoa changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji"alisema Gabriel.
Mwanamama huyo aliongeza kusema kuwa wakina mama wameteseka kwa mda mrefu huku wakifuata huduma za maji ambapo kuna baadhi ya wakina mama wameachika na wengine wakiambulia kipigo kutoka kwa wanaume zao baada ya kuchelewa kurudi nyumbani.
Gabriel alimaliza kusema kuwa huduma ya maji ikiboreshwa wakina mama wajasilia mali uchumi wao utapanda kutokana na watatumia maji kuongezeka ili kupunguza msongamano uliopo kwenye mabomba ya maji na visima huku vingine vikiwa mbali.
Naye mgombe ubunge jimbo la Tarime vijijini,Mwikwabe Mwita Waitara alisema kuwa akichaguliwa na kuwa Mbunge atahakikisha maji yanakuwepo kwa kuzingatia sera ya serikali iliyopo ya maji kumtua mama ndoo ya maji kichwani.
Farida Joel Nchagwa ambaye ni mgombea nafasi ya Udiwani kata ya Kenyamanyori katika halmashauri ya Tarime Mjini alisema kuwa wakina mama wanatumia mwendo mrefu kufuata huduma za maji hali ambayo ni moja ya kero.
Nchagwa aliongeza kuwa akichaguliwa na kuwa diwani atahakikisha anashirikiana na viongozi wa serikali pamoja na mbunge wake Kembaki kama akichaguliwa ili kuwaletea maji wananchi wa jimbo la Tarime ikiwemo kata yake ya Kenyamanyori.
0 Comments