Uongozi wa timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC umehamisha mchezo wake dhidi ya Yanga Africas ambao ulikuwa ufanyike Oktoba 25 katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam na hivyo sasa utapigwa katika Dimba la CCM Kirumba jiji Mwanza.
Hatua hiyo inatokana na kutumia nafasi ambayo ilipitishwa na Bodi ya ligi katika kikao chake cha ufunguzi wa ligi kuu Tanzania Bara ambapo ilieleza kuwa timu yeyote inaruhusiwa kucheza michezo yake miwili ya nyumbani nje ya kituo mama na hivyo kama KMC FC kutumia nafasi hiyo kupeleka mchezo huo Jijini Mwanza.
Mbali na hivyo KMC FC pia inatambua thamani ya mashabiki waliopo katika mikoa mbalimbali hapa Nchini na kwamba tunalengo la kutoa burudani kwa kila eneo ambalo tunamashabiki hivyo katika awamu hii tumeona ni muhimu kupeleka burudani hiyo kwa mashabiki waliopo mkoani humo.
“Tunafahamu kuwa tunamashabiki wengi kwenye kila mkoa, hivyo ninafasi kwa watu wa Mwanza kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kushuhudia soka safi linalochezwa na timu ya KMC FC na hivyo itakuwa ni salamu tosha kwa timu nyingine kongwe kuona ubora wa kikosi hicho.
Hata hivyo KMC FC inawasishi mashabiki na wapenzi wa timu hiyo waliopo katika mikoa ya karibu na jiji la Mwanza na maeneo mengine kujitokeza kwa wingi Oktoba 25 mwaka huu katika kuhakikisha kwamba wanakuja kushuhudia timu yao itakavyofanya vizuri na hivyo kuibuka na matokeo yenye viwango dhidi ya mchezo huo na Yanga.
0 Comments