Na Timothy Itembe Mara.
Ikiwa zimebaki siku saba kuingia siku ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Okotoba 28 mwaka huu wa kuwachagua Rais,Wabunge na Madiwani mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini Esther Matiko amesema ndoto ya kujenga gorofa ipo palepale.
Matiko amekazia kuwa ahadi hiyo aliitoa wakati akiwa anagombea hapo mwaka 2015 lakini juhudi za ujenzi huo wa gorofa ziligonga mwamba baada ya kunyimwa BOQ.
“Tarajio la ahadi ya kujenga gorofa ndani ya shule hizo likopalepale kwa sababu nimefanya andiko nimepata mfadhili kinachokwamisha ni kunyimwa tu BOQ ili ujenzi uendelee na kuokoa wanafunzi kusoma kwa zamu hali hiyo pia itapandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi”alisema Matikona .
Matiko aliongeza kusema kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge atahakikisha ndoto yake hiyo inatimia na wanafunzi wanaenda kusoma kwa mda mwafaka bila kuingia kusoma kwa zamu ambapo kiwango cha ufaulu kinashuka kutokana na sababu ya mlundikano uliopo ndani ya shule hizo.
Kwa upande wake Bashiri Selemani maarufu kama Sauti alisema kuwa ataendelea kufanya kampeni licha ya kuwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji Elias Ntiruhungwa hajampa barua ya rufaa baada ya kushinda pingamizi alilokuwa amewekewa.
Sauti aliongeza kusema kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi kama jina na picha ikiwepo kwenye baroti ya kupiga kura wapiga waende kumpigia kura ili kuwa mwakilishi wao nafasi ya udiwani ndani ya kata ya Nyamisangura kwa sababu yeye ni mtu wa maendeleo.
Sauti alifafanua kuwa amesimamia ujenzi wa shule wa msingi Bugosi na kusajiliwa na hatiamaye sasa imeanza masomo licha ya kuwa aliikuta ikiwa na vyumba 2 vya madarasa.
Naye Pamba Chacha Mwita ambaye ni mgombea udiwani kata ya Sabasaba kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema alisema kuwa pindi atakapopewa barua ya kugombea baada ya kuwekewa pingamizi wananchi wamwamini na kumchagua ili kuwawakilisha katika nafasi hiyo.
0 Comments