Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) jimbo la kigoma mjini Mh kilumbe Shaban Ng’enda amesema kuwa endapo wananchi watamchagua kuwa mbunge wao atahakikisha anajenga hospitari ya rufaa katika mkoa huo.
Akizungumza hii leo na wakazi wa mkoa wa Kigoma jimbo la Kigoma mjini mgombe huyo amesema kuwa kujenga hospitari nya rufaa ndio kipaumbele chake cha kwanza kutokana na wanachi kupata changamoto kubwa katika suala la afya.
Amesema kuwa hospitari hiyo itajengwa katika kata ya Kagera ujiji mkoani Kigoma licha ya changamoto kubwa ikiwemo wananchi wa eneo hilo kuto taka kuachia maeneo hayo kwa ajiri ya ujenzi huo kwa madai ya kuhitaji fidia jambo ambalo amesema itaweza pelekea hospitari hiyo kujengwa eneo lingine tofauti na palipokusudiwa.
Aidha amesema jambo la kujenga hospitari hiyo ni muhimu kutokana na hospitari ya mkoa ya maweni kukosa vifaa tiba kama x-ray hali inayopelekea wagonjwa wengi kupelekwa muhimbili akitolea mfano kutokea kwa ajali ya Zitto zuberi Kabwe aliepelekwa maweni kisha kupelekwa Muhimbili kwa kukosekana kifaa hicho katika hospitari ya mkoa wa Kigoma Maweni.
Aidha amewaomba wananchi wa Kigoma mjini Kumpa kura za ndio ili akawawakilishe vizuri bungeni kwa kuwasemea kero na changamoto zinazo wakumba wananchi wa Kigoma mjini.
0 Comments