F Urusi yasimamia mazungumzo ya mawaziri wa mambo ya nje wa Armenia na Azerbaijan | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Urusi yasimamia mazungumzo ya mawaziri wa mambo ya nje wa Armenia na Azerbaijan

 


Urusi iliwakaribisha mawaziri wa mambo ya kigeni wa Armenia na Azerbaijan kwa mazungumzo tofauti, wakati madola yenye nguvu duniani yakijaribu kuzifufua juhudi za kufikia makubaliano ya kudumu ya usitishwaji mapigano kuhusu jimbo la Nagorno-

Karabakh. Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov amekutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Azerbaijan Jeyhun Bayramov na mwenzake wa Armenia Zohrab Mnatsakanyan kwa mazungumzo tofauti. 

Lakini mawaziri wa nchi hizo mbili hasimu hawakuwa na mazungumzo ya ana kwa ana katika mji mkuu wa Urusi. Urusi, Marekani na madola mengine yenye nguvu wanajaribu kuzishawishi pande zote kusitisha mapigano ambayo yamewauwa mamia ya watu baada ya mikataba miwili ya kusitisha mapigano kuonekana kushindwa. 

Armenia imesema wanajeshi wake 772 na raia 36 wameuawa katika mapigano hayo. Azerbaijan imesema raia wake 63 wameuawa, lakini haijafichua hasara iliyotokea kwa wanajeshi. 

Rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev amesema wanaweza tu kusitisha mapigano wakati Armenia itajiondoa katika mkoa wa Nagorno-Karabakh. 

Waziri Mkuu wa Armenia, Nikol Pashinyan amefuta uwezekano wa suluhisho la kidiplomasia katika mgogoro huo.


Post a Comment

0 Comments