Watu wawili ambao ni Kubingwa Charles (32) na Astigaz Belibwa (30), wamenusurika kifo kwa kuungua baada ya kulipukiwa na Shoti ya umeme, mkoani Geita.
Imeelezwa kuwa kuna nyaya zilikuwa zikichezewa na vijana wawili waliokuwa wakijaribu kama zinafanya kazi kwenye msongo wa kusafirisha umeme mkubwa eneo la Mpomvu Mkoani Geita.
Daktari Kitengo Cha Dharura Hospitali Ya Rufaa Mkoani Geita amethibitisha kupokea Majeruhi hao huku akisema kuwa moja kati ya majeruhi hao mmoja alikua katika hali mbaya ambae ameungua karibia asilimia 50 ya mwili wake lakini majeruhi mmoja amehudimiwa na kuruhisiwa kwenda nyumbani.
Akizungumza mmoja wa Majeruhi jinsi tukio lilivyotokea na kusema kuwa kuna watu ambao walikua wanauchezea waya wa umeme mkubwa kwa kudhani kuwa hauna nguvu na yeye alikua karibu na eneo hilo ndipo ulipopiga shoti na kuwajeruhi
Baadhi ya mashuhuda wanaelezea jinsi walivyoshuhudia ajali hiyo huku wakiwaomba wamiliki wa viwanda vya kunchenjua dhahabu kutoweka vifusi vya mchanga wa dhahabu karibu na maeneo hatarishi.
Kwa upande wake, Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Geita Fidelis Wambura, amesema wameshirikiana na wananchi kuwanasua wafanyakazi hao walionaswa kwenye umeme na kuwakimbiza hospitali huku akitoa wito kwa wamiliki wa viwanda vya kuchenjua dhahabu kuwa makini na kurundika mchanga wao katika maeneo hatarishi.
0 Comments