Urusi imeunda vifaru vipya ambavyo vimeifanya Norway kuanza kufikiria upya mfumo wake wa kukabiliana na vifaru wakati wa vita.
Vifaru hiyo vipya vya Urusi kwa jina Armata T-14 vinaundwa vikiwa na teknolojia ya Kinga Dhidi ya Makombora (APS).
Lengo la teknolojia hiyo ni kuwezesha vifaru hivyo kutoharibiwa na makombora mengi yaliyoundwa kukabiliana na vifaru, yakiwemo yale aina ya Javelin yanayoundwa Marekani, ambayo yanatumiwa na jeshi la Norway.
Brigidia Ben Barry wa taasisi kuhusu usalama wa kimataifa ya International Institute for Strategic Studies (IISS) mjini London anasema mataifa yanafaa kuanza kufikiria upya mifumo ya kukabiliana na makombora.
Anasema mataifa mengi ya Shirika la Kujihami la nchi za Magharibi (Nato) hayajagundua tatizo linalowakabili.
Teknolojia ya APS inatishia kufanya silaha nyingi za kukabiliana na vifaru kutofanikiwa, na mataifa mengi ya Magharibi hayajaanza kujadiliana na kubadilisha mawazo kuhusu hatua za kuchukua.
Anasema baadhi ya nchi zinafanya utafiti na majaribio kivyake kuweka mfumo huo wa APS kwenye vifaru vya mataifa hayo.
"Lakini yanakosa kuzingatia matokeo ya teknolojia hii kwa mfumo wao wa kukabiliana na vifaru," anasema.
Norway ni moja ya nchi za kwanza kukumbana na hatari hii.
Nchi hiyo inapanga kutumia krona 200-350 milioni (£18.5-32.5 milioni; $24-42 milioni) kubadilisha makombora yake ya Javelin na "kudumisha uwezo wake wa kukabiliana na vifaru".
"Kuna haja ya kuwa na makombora ambayo yanaweza kupinga mfumo wa APS."
Teknolojia ya APS imebadilisha mambo katika historia ya kuangazia kushambulia na kujilinda wakati wa vita.
Katika vipindi fulani, kuna moja ambayo imekuwa mbele.
Zamani, vifaru visivyoweza kupenya risasi vilitawala, lakini makombora nayo yakaimarishwa na kumaliza ubabe huo.
Tangu Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, vifaru vimeendelea kutawala katika uwanja wa vita.
Vifaru hata hivyo, huwa vinaweza kuharibiwa na makombora au mabomu ya vifaru vingine vikiwa karibu.
Lakini kulikuwa pia na tishio kutoka kwa silaha nyingine, mfano makombora ya kurushwa kutoka mbali au kutoka kwa ndege, jambo ambalo ndilo teknolojia ya APS imeundwa kukabili.
0 Comments