F Mbunge wa jimbo la Lindi aiomba TARURA itengeneze maeneo korofi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mbunge wa jimbo la Lindi aiomba TARURA itengeneze maeneo korofi


Na Ahmad Mmow, Lindi.

Mbunge wa Lindi mjini, Hamida Abdallah licha ya kupongeza juhudi za Wakala wa barabara za mijini na Vijiji ( TARURA) wa halmashauri ya manispaa ya Lindi itengeneze maeneo korofi yaliyo kwenye barabara zilizopo katika jimbo hilo.

Mheshimiwa Hamida alitoa wito huo jana alilotembelea Ofisi ya Wakala huo zilizopo manispaa ya Lindi, ikiwa ni mwendelezo wa ziara anayofanya jimboni humo.

Alisema TARURA imekuwa na jitihada kubwa katika kutimiza wajibu wake. Hata hivyo hainabudi kufanyia matengenezo maeneo korofi ya barabara

ambazo baadhi yake hazipitiki vipindi vya mvua. Hali inayosababisha wananchi wa baadhi ya maeneo kushindwa kupata huduma za msingi kwa wakati.

Mbunge huyo alisema kabla na baada ya uchaguzi, hasa kipindi cha kampeni alitembelea mitaa yote iliyopo katika manispaa ya Lindi, na kubaini kwamba baadhi ya barabara ni mbovu zinazohitaji matengenezo ya haraka kabla ya mvua za masika kuanza.

" Baadhi ya maeneo korofi mmetengeneza, nawapongeza sana. Lakini pia nambua suala la ufinyu wa bajeti. Hata hivyo baadhi ya barabara zina maeneo korofi naomba myape kipaumbele. Na barabara nyingine ziwekeni kwenye mpango," alisema mbunge Hamida.

Alisema barabara nikichocheo cha uchumi kwa wananchi. Hata hivyo kushindwa kupitika kwa nyakati zote kunasababisha kupunguza kasi ya wananchi kufanya Kazi za kiuchumi na maendeleo.

" Kuna baadhi ya barabara ukiwa na viatu vyenye uzito wa nusu kilo huwezi kunyanyua kutokana na tope, gari haziendi na hata bodaboda wanakataa kwenda, kwa mfano barabara ya Jangwani. Kwahiyo wananchi wanapata tabu na wanishindwa kupata huduma na mahitaji muhimu kwa wakati. Lakini pia ile ya Kineng'ene kwenda Chikonji ni muhimu ikawekwa kwenye mpango wa kiwango cha lami. Ingawa mpango siyo utekelezaji na kata zote zina changamoto," alisitiza.

Alisema barabara  ya Mtange- Chikonji ilikuwa na changamoto. Hata hivyo TARURA imefanyia matengenezo, ingawa  bado kwenye barabara kuna eneo linahitaji kufanyiwa kazi. Kwani lina kona kali na iwapo kutakuwa na uwezekano ijengwe daraja. Huku akiitaja barabara ya Nyipiti- Kineng'ene kuwa ni miongoni mwa barabara zinazohitaji matengenezo.

Alizitaja barabara nyingine kuwa ni Nabiriki. Kwani mbovu kiasi cha wananchi kuwa tayari kujitolea kuchimba miti ili kupanua barabara hiyo ambayo hazipitiki. Lakini pia aligusia barabara za Rahaleo, Ndolo, Kitunda na Nachingwea kuwa zinahitaji kufanyiwa matengenezo.

Mbali na hayo alitoa wito kwa taasisi hiyo isimamie kikamilifu sheria ili kudhibiti uharibifu wa miundo mbinu na wizi wa vifaa

na alama za barabara. Akibanisha kwamba sheria zipo bali tatizo ni usimamizi na utekelezaji wa sheria hizo.

Kwaupande wake, meneja wa TARURA wa halmashauri ya manispaa ya Lindi, mhandisi Lusekelo Mwakyoma licha ya kueleza mafanikio na changamoto wanazokutana nazo alisema TARURA inaandaa njia nzuri ya kuwadhibiti waharibifu wa miundo mbinu na wezi wa alama za barabarani ambayo itawafanya wakamatwe kirahisi.

Post a Comment

0 Comments