F Mwenyekiti halmashauri ya wilaya Tarime alazimika kuunda tume ya uchunguzi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mwenyekiti halmashauri ya wilaya Tarime alazimika kuunda tume ya uchunguzi


MWENYEKITI alazimika kuunda Tume ya watu watatu kwenda kuchunguza magari mawili na Trekta moja baada ya utata kuibuka ndani ya Baraza la madiwani wa halm,ashauri ya Tarime wilaya na kurejesha taarifa sahihi.

Baraza hilo lilikuwa na lengo la kujadili taarifa ya utekelezaji shugili za miradi wakati ambapo baraza lilikuwa limevunjwa ambayo iliandaliwa na mkurugenzi Apoll Tindwa lilokalia katika ukumbi wa shule ya sekondari JK Nyerere uliopo Nyamwaga ambapo kikao hicho kiliongozwa na mwenyekiti wake Simon Kiles Samwel. 

  Kamati ya madiwani watatu iliyoundwa na mwenyekiti huyo ni pamoja na Amos Sagara Nyabikwi [Sirari], John Muhabasi [Nyarero] na Mariam Mkono [ viti maalum Ingwe] waliokwenda hadi karakana ya Peter Makoba iliyopo katika Ardhi ya Halmashauri ya mji wa Tarime kubaini uwepo wa   magari ya SM 5142, SM 5241 na Trekta SM 9396  kwa ajili matengenezo.

 Hatua hiyo ilijitokeza baada ya madiwani hao kupatwa na mashaka ya taarifa ya Mkurugenzi wa  Halmashauri Apoo Castro Tindwa  yake ya Julai hadi oktoba mwaka huu kulipovunjwa baraza madiwani waliomaliza muda wao walipopokea, pitia na kujadili madiwani wa baraza jipya taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kipindi hicho. 

Kaimu mkurugenzi ambae ni mkuu wa Idara ya  mipango wa Halmashauri hiyo Frederick Mallya  alishindwa kutetea hoja  kutbibitishia na watalaam wake mbele ya  madiwani katika kikao cha siku hiyo idadi kamili ya magari mabovu ni 9 na trekta 1 au 6 na trekta 1 baada ya taarifa za mkanganyo huo kuonekana idadi hizo mara mbili katika kablasha la mkurugenzi Tindwa.

 Aidha Taarifa ya Mkurugenzi Tindwa ilishindwa katika kablasha hilo kubainisha wazi licha ya kukanganya idadi mbili tofauti za mali hizo za Halmashauri zilipoandikwa kuwa ni mbovu kila gari haikuoneshwa ubovu wake, gharama zinazotumika za mafundi matengenezo yake, na yalipo katika karakana na muda yalipoingizwa kwenye matengenezo yake.

Madiwani katika baraza hilo walipohoji kujua magari hayo yalipo, na mmiliki wa karakana inayotengeza magari hiyo ni nani na kuutaka uwekwe wazi mktaba wake wa matengenezo wa  magari ya Halmashauri hiyo Kaimu mkurugenzi huyo Mallya alisema kuwa jina na mkataba wa matengenezo yake  ya mmiliki wa karakana hiyo upo na utaletwa kwenye kamati ya mipango, fedha na uongozi ulioonesha mchanganuo wote ukihitajika.

Timu ya madiwani watatu walioongozwa na diwani machachari wa viti maalum tarafa ya Ingwe Mariam Mkono baada ya kufika na kufanya uchunguzi wake iliwasilisha taarifa yake katika baraza la madiwani hao mbele ya mwenyekiti wao Simon Kiles Samwel, kuwa  gari SM 5142 halipo kwenye karakana ya Peter Makoba.

Waliendelea kuweka wazi kuwa gari SM 5241 walilikuta lipo kwenye matengezo yake tangu liingizwe kwenye karakana hiyo oktoba 26 mwaka huu baada ya kufanya safari za shughuli za Halmashauri hiyo maeneo mbali mbali na kuharibika PUMP ambayo mmiliki wa karakana hiyo aliwaambia kuwa PUMP hiyo iliagizwa kutoka mwanza ndiyo inasubiliwa kukamilisha matengenezo yake.

Waliendelea kuweka wazi kuwa trekta SM 9396 la kilimo lilikutwa katika karakana hiyo likiwa tayari limeisha kamlika matengenezo yake linasubiliwa kufatwa ama kutekeleza mkataba wa malipo yake  kuwa mikononi mwa Halmashauri hiyo.

Baada ya kutolewa taarifa hiyo  na timu hiyo madiwani walimhoji kaimu Mkurugenzi Mallya kujua gari SM 5142 karakana lililopo baada ya kutoonekana na karakana ya Peter Makoba , ndipo alisema gari hilo lipo karakana moja ambayo hakuweza kuitaja katika jijini mwanza likiendelea na matengenezo huku akishindwa kuweka wazi ubovu wake ni upi.

Kutokana na utata huo, mwenyekiti wa Halmashauri hiyo alitangaza kuwa mkanganyo wa idadi ya magari hayo mabovu na mazima likiwemo trekta moja  na sambamba na kule kulikobainika mashaka katika  taarifa kutoka katika idara mbali mbali za Halmashauri hiyo  Mkurugenzi Tindwa hana budi kuwasilisha taarifa  pia za  mali za nyumba zilizopo katika Ardhi ya Halmashauri ya mji  kuzibaini kwenye kamati ya Fedha, Mipango na Uongozi kupitiwa, kujiridhisha na kujadiliwa na baadae kurejshwa katika kikao cha baraza la madiwani.

Wakati huo huo diwani wa viti maalum tarafa ya Inchage katika kata ya Nyarero Robi Mwita alihoji kujua iweje mmoja wa maafisa ushirika ambae alimtaja jina lake katika kikao cha baraza hilo la madiwani siku hiyo kuwa alikusanya fesha za wanavikundi viwili vya jumla ya akina mama 60 kila mmoja shilingi 20, 000 aliyedai kuwa  fedha hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kuwakatia vitambulisho kila mmoja vya ujasilia mali  vilivyotolewa na Rais Dk John Pombe Magufuli na kisha kuishia kusikojulikana hadi leo wanasubilia akina mama hao.

Diwani huyo alisema kuwa mtumishi huyo aliwaminisha wana vikundi hivyo vilivyopo katika kijiji cha Kemakorere kuwa angeliwarejeshea vitambulisho hivyo kila mmoja kwa muda mfupi  baada ya kupewa fedha hizo zaidi ya milioni 1 lakini hadi sasa hajafanya hivyo.

Mbali na diwani huyo kuhoji hivyo, pia diwani wa viti maalum tarafa ya Ingwe kata ya Nyamwaga aliweka wazi juu ya adha wanazozipata akina mama waliokwenda kwa ofisi ya maendeleo ya jamii kuomba mikopo isiyo kuwa na riba kutokana na kile alichokidai diwani huyo kuwa wanaombwa rushwa na ambao wanashindwa kutekeleza hivyo  hawafanikiwi mikopo hiyo.

Mkono alisema kuwa kutokana na changamoto hiyo akina mama wengi kupitia vikundi vyao wamekata tamaa ya kufanikiwa kupata mikopo hiyo waweze kujikwamua na lindi la umasikini  ambapo Halmashauri hiyo ilitenga asilimia 10 ya vikundi vya kijamii, asilimi 4 akina mama, asilimia 4 ni vijana na asilimia 2 ni walemavu.

Madiwani waliomba maafisa wanaohusishwa na rushwa kuwakwaza akina mama hao kushindwa kufanikiwa mikopo wachunguzwe kwa kile walichoeleza kuwa ni kinyume cha maadili ya utumishi wa umma na pia ni kinyume cha sheria za nchi na kisha wakibainika wachukuliwe hatua za kimaadili na kisheria.

Pamoja na maauzi ya madiwani hao mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Samwel alitangaza kuwa malalamiko hayo yanawasilishwa  kwenye kikao cha kamati ya fedha, mipango na utawala ili kupitia mambo mbali mbali  ya utekelezaji wa idara yake Afisa maendeleo wa Halmashauri hiyo ikiwa ni pamoja na kujibu tuhuma hizo ikibainika  kuna ukwel ndani mwake.

Katika kikao cha baraza la madiwani hao kilichoketi desemba 21, 2020 kiliamuliwa kuketi baada ya madiwani wa baraza hilo desmba 15 mwaka huu kukataa kuipoke, kupitia na kisha kuijadili na kisha kutolea maamuzi yao taarifa ya mkurugenzi Apoo Castro Tindwa  siku hiyo ya Julai hadi oktoba 2020 ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo wakati madiwani wa sasa hawakuwepo kwa kile ambacho kilibainika kuwa mkurugenzi huyo alikyuka kanuni ya kudumu ya Halmashauri hiyo iliyo mtaka awasilishie makblasha kabla ya siku saba wapate kusoma.


Post a Comment

0 Comments