Nyota wa muziki nchini, The African Princess Nandy ameweka wazi kuwa ametolewa barua ya posa, hivyo kinachofuata ni kuolewa.
Katika ujumbe ambao ameuposti kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nandy amedokeza hilo kwa kifupi. “Nimepokea ujumbe, barua yake imepokelewa nyumbani…… (wife to be ),” ameandika Nandy.
Ikumbukwe #Nandy tayari amevishwa pete ya uchumba na rapa @billnass mapema mwaka huu. Kwa sasa wawili hao wanafanya vizuri na wimbo wao "Do Me"
0 Comments