F Umoja wa Ulaya na Uingereza zapata muafaka wa biashara | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Umoja wa Ulaya na Uingereza zapata muafaka wa biashara

 



Baada ya miezi kumi ya mazungumzo, hatimaye Uingereza na Umoja wa Ulaya zimefikia makubaliano ya kibiashara, yanayowazesha kuulainisha mtikisiko wa kiuchumi unaotakana na Uingereza kujiondowa kwenye Umoja huo. 


Kwa mujibu wa makubaliano hayo yaliyotangazwa jioni ya jana, wakati Uingereza itakapoondoka kwenye soko la pamoja la Ulaya katika Mkesha wa Mwaka Mpya, haitakabiliwa na vikwazo vya ushuru wa forodha kwa biashara inayofanyika kupitia bahari. 


Akitangaza makubaliano hayo, Waziri Mkuu Boris Johnson amesema wamefanikiwa kurejesha udhibiti wa sheria zao na pia mustakabali wao kikamilifu na kwa mujibu wa uamuzi wa Waingereza. 


Kwa upande wake, Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, amesema licha ya furaha ya kuhitimisha mazungumzo kwa mafanikio, lakini kutengana kwa Umoja huo na Uingereza ni jambo la huzuni.

Post a Comment

0 Comments