Habari za muda huu mpenzi msomaji wa blog hii ya Muungwana bila shaka u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku.
Naomba nichukue walau sekunde chache kama si dakika kadhaa kukuweza kukueleza ni kwa namna ambavyo utaweza kutengeneza cripsi kwa kutumia viazi mviringo.
Crips hizi unaweza kutengeneza kwa ajili ya biashara lakini vile vile kwa ajili ya ya kula pamoja na familia yako.
Sasa naomba twende tukaone moja kwa moja mahitaji ya kutengeneza cripsi kama ifuatavyo:
1. Viazi kilo 1
2. Mafuta lita moja.
3. Chumvi kijiko kias
4. Pilipili ya unga kijiko kimoja (hii inategemeana kama unataka kuweka)
5. Ndoo
6. Beseni
7. Upawa wa kukaangia wenye matundu
8. Bakuli yenye matundu/kitaulo safi
9. Kikaangio
10. Jiko
Namna Ya Kutengeneza
Menya viazi vyako, osha na ukatekate sles ndogondogo kisha weka kwenye beseni weka chumvi na viache vikauke maji.
Washa jiko na uweke chungu chako cha kukaangia weka mafuta yaache yachemke uweke vipande vyako vya viazi viache mpaka viwe brown ya mbali kisha chukua upawa wako wenye matundu na uipue weka kwenye bakuli la kuchujia mafuta kisha weka pilipili tayari kwa matumizi.
Kwa mahitaji ya masomo kama haya endelea kufatilia blog hii kila wakati.
Imeandikwa Na Benson Chonya.
0757909942
Bensonchonya23@gmail.com
0 Comments