F Wasichana 55 walioepushwa na ukeketaji warejeshwa kwa wazazi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wasichana 55 walioepushwa na ukeketaji warejeshwa kwa wazazi

 


Watoto wa kike 55 waliokuwa wamehifadhiwa katika Kituo cha Hope For Girls and Women Tanzania kilichoko Mugumu Serengeti kwa kukimbia kukeketwa wanatarajiwa kurejeshwa kwao baada ya kukamilika taratibu za kiserikali.


Kila mwaka unaogawanyika kwa mbili kabila la Wakurya hukeketa watoto wa kike na tohara ya kienyeji kwa wavulana, baadhi yao wasiokubali hukimbilia polisi, makanisani na nyumba salama.


Mkuu wa Kituo cha Hope, Daniel Misoji leo Jumamosi Januari 9 ameiambia Mwananchi kwa simu kuwa shirika hilo kwa kushirikiana na dawati la polisi na Ustawi wa Jamii wanatarajia kuwarejesha watoto hao kwao ili waendelee na masomo kuanzia Januari 11 mwaka huu.


"Kwa kipindi cha Desemba 2020 tulipokea watoto 55 waliokimbia ukeketaji ambao leo baada ya kuwa tumeishajenga mahusiano na wazazi kupitia viongozi wa vijiji na tunatarajia kuwarudisha kwao ili waendelee na masomo yao," amesema.


Mkurugenzi wa shirika hilo Rhoby Samwel amesema shirika hilo huwatunza watoto kwa niaba ya serikali kwa kuwa wanapitia taratibu zote na wakati wa kuwarudisha serikalini ili kuweka utaratibu mzuri na wazazi chini ya uangalizi wa viongozi wa vijiji wasije kuwafanyia ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji.

Post a Comment

0 Comments