F Chombo cha anga za juu cha Perseverance rover cha Nasa chatua sayari ya Mihiri. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Chombo cha anga za juu cha Perseverance rover cha Nasa chatua sayari ya Mihiri.


Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) limefanikiwa kuwezesha kutua salama kwa chombo chake cha Perseverance rover katika bonde kubwa lenye kina yaani kreta karibu na ikweta ya sayari hiyo inayojulikana na Jezero.

"Taarifa njema ni kwamba chombo hicho cha anga za mbali kiko katika hali nzuri," amesema Matt Wallace, naibu meneja wa mpango huo.

Wahandisi wa Nasa waliokuwa wanadhibiti chombo hicho huko California walijawa na furaha isiyokifani walipothibitisha kwamba chombo cha Perseverance rover kimetua salama salmini katika sayari ya mihiri.

Chombo hicho chenye magurudumu 6 sasa kitakuwa kwenye sayari hiyo kwa takriban miaka miwili katika mabonde ya eneo hilo, kikitafuta ushahidi unaonesha shughuli za maisha ya awali.

Ikweta ya Jezero inadhaniwa kwamba imekuwa na ziwa kubwa kwa miaka bilioni kadhaa iliyopita.

Na mahali ambapo kumekuwa na maji, kuna uwezekano mkubwa kulikuwa na maisha yalioendelea eneo hilo.

Post a Comment

0 Comments